Hali ambayo maiti aliyekufa atalazimika kulipa na hali ambayo hatolazimika

Swali: Mtu akifa hali ya kuwa yuko juu yake na siku za Ramadhaan au nadhiri familia yake wamfungie au wamtolee kafara badala ya kumfungia?

Jibu: Ikiwa alipona na akaweza kufunga lakini hata hivyo akafa kabla ya kufunga imesuniwa kwa ndugu zake kumfungia. Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:

“Atakayekufa na juu yake yuko na swawm basi walii wake amfungie.”[1]

Walii ni yule mtu wa karibu kama vile baba, mtoto, binadamu na wengineo.

Ikiwa maradhi yake yaliendelea mpaka akafa basi si yeye wala ndugu zake hawalazimiki kulipa wala kutoa fidia.

[1] al-Bukhaariy (02/240), Muslim (02/803), Ahmad (06/69) na wengineo.

  • Mhusika: al-Lajnah ad-Daaimah
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Fataawaa al-Lajnah ad-Daaimah (10/328-329)
  • Imechapishwa: 18/06/2017