Swali: Kuna mtu alijiunga na imamu katika Rakaa ya kwanza. Wakati imamu alipokaa katika Tashahhud ya kwanza akakaa naye. Pindi imamu aliposimama katika Rakaa ya tatu maamuma huyu hakumsikia isipokuwa mpaka baada alipokuwa amefika katika Rukuu´. Hivyo akawa amesimama moja kwa moja na akaenda naye katika Rukuu´. Ni ipi hukumu ya swalah yake?

Jibu: Swalah yake ni sahihi. Kuchelewa kwake ni kwa sababu ya udhuru; hakumsikia imamu. Maadamu amewahi Rukuu´ hahitajii kusimama na kusoma kwa sababu ni mwenye kupewa udhuru.

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh Tafsiyr-ish-Shaykh Muhammad bin ´Abdil-Wahhaab (12) http://www.alfawzan.af.org.sa/sites/default/files/tf–1432-08-02.mp3
  • Imechapishwa: 29/05/2018