Hakutazamwi nia ya mtamkaji talaka isipokuwa ya kinaya

Swali: Ikiniteleza nikaapa kwa asiyekuwa Allaah pasina kukusudia, je mimi nitakuwa mwenye madhambi kwa hilo? Na lipi ni kubwa; kufanya hivyo au Zinaa na kunywa pombe?

Jibu: Mwenye kufanya hivyo kakusudia kuapa kwa Talaka (na si kwa asiyekuwa Allaah). Mtu akiapa kwa Talaka, je Talaka inapita au inakuwa ni juu yake kafara ya yamini? Wanachuoni wengi wanaona kuwa, mtu akiapa kwa Talaka inapita. Shaykh-ul-Islaam bin Taymiyyah na kundi na wanachuoni wenye kuhakiki wanasema kuwa haipiti kwa kuwa hii ni kama yamini. Ni juu ya aliyefanya hivyo kutoa kafara (ya yamini). Anasema Allaah (Ta´ala):

قَدْ فَرَضَ اللَّـهُ لَكُمْ تَحِلَّةَ أَيْمَانِكُمْ

“Allaah Amekwishakufaridhishieni (nyinyi Waislamu Shari’ah) ya kufungua viapo vyenu.” (66:02)

Aayah hii ni kwa jumla, kuapa kwa asiyekuwa Allaah na kuapa kwa Talaka. Ni juu yake kutoa kafara na wala Talaka haipiti. Kwa kuwa hakukusudia Talaka, isipokuwa amekusudia yamini. Namna hii ndivyo walivyotofautiana. Lakini kauli ya salama ni kuwa Talaka inapita. Ikiwa ni Talaka rejea, atamrejea mke wake. Na ikiwa sio Talaka rejea, ameharamika kwake. Hii ndio kauli iliyo ya salama. Ama wanaosema kuwa hakukusudia hivyo, Talaka haikushurutishwa nia. Mtu akitamka Talaka, hakukushurutishwa nia. Akiitamka inapita. Hata ikiwa atadai kuwa hakukusudia hivyo. Sisi hatutazami nia yako bali tunachotazama ni matamshi yako. Nia inatazamwa tu katika hali ya kinaya, lau atatamka lafdhi ya kinaya na kusema mimi sikukusudia hivyo na lafdhi yenyewe ikawa ya kinaya, hapo ndo atabainisha katika hili. Ama mtu akitamka Talaka ya wazi, sisi hatutazami nia yake.

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: http://www.alfawzan.af.org.sa/node/10042
  • Imechapishwa: 04/03/2018