Hakuna yeyote anayeitwa msemezwa na Allaah (كليم الله ) isipokuwa Muusa pekee

Swali: Je, mtu anaweza kusema kuwa ´Abdullaah Ibn Haraam (Radhiya Allaahu ´anh) ni kaliymu [msemezwa na] Allaah?

Jibu: Hapana. Hili ni jambo maalum kwa Muusa (´alayhis-Salaam). Hata Mtume wetu mtu hawezi kusema kuwa ni msemezwa na Allaah na kuwa Allaah alimzungumzisha usiku wa Mi´raaj. Mtu hawezi kusema kuwa ni msemezwa na Allaah. Hili ni jambo maalum kwa Muusa (´alayhis-Salaam).

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh Zaad-il-Ma´aad (48) http://www.alfawzan.af.org.sa/sites/default/files/mo–1432-04-15.mp3
  • Imechapishwa: 16/11/2014