Hakuna yeyote amekwishamuona wala kumsikia al-Mahdiy wa Raafidhwah

Raafidhwah wanadai kwamba kiongozi wao wa zama hizi aliyejificha na anayesubiriwa Muhammad bin al-Hasan aliyeingia ndani ya pango la Saamurraa takriban mwaka wa 260. Kipindi hicho alikuwa bado hajakuwa na uwezo wa kupambanua mambo. Alikuwa ima na miaka miwili, mitatu au mitano. Kwa mujibu wao hivi sasa atakuwa na zaidi ya miaka mia nne. Hakuna yeyote aliyemwona au kuona athari yake. Hakuna yeyote aliyesikia chochote kutoka kwake. Hakuna yeyote anayemjua si kwa kumuona wala kupitia sifa zake. Pamoja na hivyo wanasema kwamba mtu huyu, ambaye hakuna yeyote amekwishamuona wala kusikia khabari zake, ndio kiongozi wa zama zao.

  • Mhusika: Shaykh-ul-Islam Ahmad bin Taymiyyah
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Minhaaj-us-Sunnah an-Nabawiyyah (1/113-114)
  • Imechapishwa: 16/12/2018


Takwimu
  • 25
  • 413
  • 1,821,444