Hakuna wanachuoni Salafiyyuun katika mji wako? – Haya ndio unayotakiwa kufanya

Swali: Ni zipi nasaha zako kwa mwanafunzi ambaye anaishi katika nchi ambayo haina wanachuoni katika Ahl-us-Sunnah na badala yake Ahl-ul-Bid´ah kama vile Ibaadhiyyah ndio wengi.

Jibu: Ni wajibu kwako kuwauliza wanachuoni, kuwapigia simu na kusoma vitabu vya Ahl-us-Sunnah. Anatakiwa kusafiri kwenda kutafuta elimu kila wakati anapoweza. Asafiri kwenda katika miji ambayo ina wanachuoni, apige goti chini yao na afaidike kutoka kwao. Vilevile asome kutoka kwenye vitabu vyao na mikanda yao. Kwa hayo Allaah (Subhaanahu wa Ta´ala) atamsaidia.

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: https://www.youtube.com/watch?v=oMoaMLGx4k0
  • Imechapishwa: 09/12/2017