Swali: Je, ni mtawala peke yake ndio anafaa kuwapiga vita kundi lenye kukataa kutekeleza Shari´ah za Kiislamu za dhahiri?

Jibu: Vita zote zinatokamana na mtawala. Haijuzu isipokuwa kwa mtawala. Vita pasi na mtawala ni vurugu. Sio vita katika njia ya Allaah. Allaah hakutuamrisha hili. Hata wana wa Israaiyl walimwambia Mtume wao:

ابْعَثْ لَنَا مَلِكًا نُّقَاتِلْ فِي سَبِيلِ اللَّـهِ

“Tutumie mfalme tupigane katika njia ya Allaah.” (02:246)

Waliomba kiongozi ambaye atawaongoza katika Jihaad. Hawakuchukua silaha na kila mmoja akaenda njia yake:

ابْعَثْ لَنَا مَلِكًا نُّقَاتِلْ فِي سَبِيلِ اللَّـهِ

“Tutumie mfalme tupigane katika njia ya Allaah.”

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh Fath-il-Majiyd (26) http://www.alfawzan.af.org.sa/sites/default/files/fathul%20%20-%204%20-%201%20-%201436.mp3
  • Imechapishwa: 11/02/2017