Enyi waislamu! Mcheni Allaah juu ya nafsi zenu wenyewe na kwa watoto wenu. Ninaapa kwa Allaah ya kwamba ikiwa wengine watapewa udhuru basi nyinyi hamtopewa udhuru kwa hali yoyote kwa sababu haki iko mbele yenu na mnaisoma katika shule za msingi, sekondari, vyuo vikuu, shahada ya pili na ya tatu. Vitabu vya Ibn Taymiyyah, Ibn-ul-Qayyim, Ahmad bin Hanbal na al-Bukhaariy mko navyo. Uko wapi udhuru wenu? Isitoshe vitabu hivyo mnavifahamu.

Enyi mahakimu wa Kiislamu! Semeni neno la haki. Enyi wanafunzi! Mnusuruni Allaah na Yeye atakunusuruni. Msiwanusuru watu wa upotevu na wala msiwanusuru Ahl-ul-Bid´ah. Fuateni mfumo wa Imaam Ahmad ambaye hakunyamazia suala hata moja. Imaam Ahmad alikuwa yuko tayari kujitolea heshima na damu yake. Ahl-us-Sunnah walipingana naye na damu ikamwagwa kwa sababu ya suala moja miongoni mwa masuala ambayo Sayyid Qutwub pia yuko nayo. Ahmad alikuwa tayari kujitolea nafsi yake kufa.

Ahl-us-Sunnah walijitolea nafsi zao wakaziweka khatarini kwa ajili ya msemo wa kusema kuwa Qur-aan imeumbwa. Ninaapa kwa Allaah ya kwamba Sayyid Qutwub pia anasema msemo huu. Kadhalika amesema Wahdat-ul-Wujuud, akaisapoti na kuisifu katika mashairi na nathari yake. Hakuna anayepinga haya isipokuwa mtu ambaye hamwogopi Allaah (Tabaarak wa Ta´ala) na hamchi Allaah juu ya waislamu. Alisema ujamaa na Haakimiyyah. Alisema nini kuhusu Haakimiyyah? Alisema ni lazima Uislamu uhukumu. Kwa nini? Kwa sababu Uislamu ni ´Aqiydah moja yenye kukubaliwa ambayo ndani yake mna mchanganyiko wa ujamaa [socialism] na umasoni kikamilifu na ndani yake kunapatikana malengo yote hayo mawili. Ukiongezea juu ya hayo mawili kwenye Uislamu kuna msimamo na usamehevu! Alisema namna hii ya kwamba Uislamu unakubaliana na ukomunisti na unaswara kwa uchanganyifu mkamilifu ambapo ndani yake mnapatikana malengo yote hayo mawili, bi maana malengo ya ukomunisti na unaswara. Kwa mujibu wake yeye anaonelea kuwa Muhammad alitumwa kuhakikisha ukomunisti na unaswara! Mustashirik waliosema kuwa Muhammad ameichukua Qur-aan kutoka kwenye Tawraat na Injiyl hawakufikia kusema upotevu kama huu. Anataka kusema kuwa Uislamu umechukua kutoka kwenye ukomunisti na unaswara. Au uhakika wa mambo Uislamu umepiga vita ukomunisti na unaswara. Huku ni kuuhujumu Uislamu namna gani.

  • Mhusika: ´Allaamah Rabiy´ bin Haadiy al-Madkhaliy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Kutoka kitabu “Firqat-un-Naaniyah – Misingi na I´tiqaad zake”
  • Imechapishwa: 27/08/2020