Swali: Je, kuna tofauti kati ya zinaa na Tahliyl[1]? Lipi baya zaidi? Je, mtu anapigwa mawe kwa ajili ya Tahliyl?

Jibu: Hakuna tofauti kati ya hayo mawili. Ni uzinzi. Hakuna tofauti kati ya zinaa na Tahliyl kwa sababu ndoa hiyo haina maana yoyote. Kwa hiyo ni jimaa isiyokuwa na sababu ya kuihalalisha.

[1] Imaam Ibn Baaz (Rahimahu Allaah) amesema:

”Ndoa nyingine iliyoharamishwa na Allaah (´Azza wa Jall) na imetokea kwa baadhi ya watu ni ndoa inayoitwa “kufanya halali”, Tahliyl. Pindi mwanamume anapomtaliki mke wake kwa mara ya tatu na hivyo anakuwa hawezi kumrudi tena, anakubaliana na mwanaume mwingine ili amuoe. Pindi yule mume wa pili anapomuoa na kumwingilia, anamtaliki ili aweze kurudi kwa yule mume wake wa kwanza. Hii ndio ile ndoa inayoitwa “Tahliyl” na inafanywa na watu wenye imani dhaifu na wasiomcha Allaah (´Azza wa Jall). Imethibiti kutoka kwa Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) ambaye amesema:

“Allaah amlaani yule mwanaume anayefanya halali na yule mwanaume anayehalalishiwa.” (Ibn Maajah (1963). Nzuri kwa mujibu wa al-Albaaniy katika ”Swahiyh Sunan Ibn Maajah” (1585)) http://www.alifta.net/Fatawa/FatawaChapters.aspx?languagename=ar&View=Page&PageID=3998&PageNo=1&BookID=4

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh Ighaathat-il-Lahfaan (58) http://alfawzan.af.org.sa/sites/default/files/15-01-1438-ighastat.mp3
  • Imechapishwa: 22/10/2017