Kusikizwa na kutiiwa ni haki mbili za kiongozi au mtawala. Usikivu na utiifu ni katika matunda ya bay´ah. Kwa kuwa bay´ah ni fungamano na ahadi ya usikivu na utiifu. Bay´ah inapatikana ima moja kwa moja au kwa niaba.

Kundi la wanachuoni na Ahl-ul-Hall wal-´Aqd wakimpa bay´ah kiongozi wa waislamu basi inatakiwa kutokana na bay´ah hiyo waislamu wengine wote wawafuate kwa kumsikiliza na kumtii. Namna hii ndivyo ilivokuwa Sunnah ya Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) na Sunnah ya makhaliyfah wake waongofu.

Hakuna tofauti kati ya usikivu na utiifu [kwa mtawala] na bay´ah. Yule mwenye kutofautisha kati ya usikivu na utiifu katika haki ambazo ni za kiongozi wa waislamu au mtawala wa waislamu, hana dalili ya hilo kutoka kwenye Sunnah za Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) wala matendo ya Maswahabah na Taabi´uun wala maneno ya Ahl-us-Sunnah wal-Jamaa´ah na wafuasi wa wema waliotangulia katika ´Aqiydah yao.

  • Mhusika: Shaykh Swaalih bin ´Abdil-´Aziyz Aalush-Shaykh
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh al-Arba´iyn an-Nawawiyyah, uk. 382
  • Imechapishwa: 13/05/2020