Hakuna tabasamu kwa Ahl-ul-Bid´ah na watu wa Maulidi

Swali: Vipi mtu anatakiwa kutangamana na Ahl-ul-Bid´ah na kwenda kwao kinyuma wanaposema kwamba ni sawa kusherehekea mazazi ya Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam)?

Jibu: Ni wajibu kwa mtu kujiepusha na watu hawa. Jambo la kwanza mtu anatakiwa kuwanasihi ikiwa unaweza kufanya hivo. Wasipokubali basi jitenge nao mbali. Ikiwa huwezi kuwapa nasaha basi jiepushe nao na wala usikae nao na wala usiwazungumzishe. Ikiwa umelazimika kuitikia salamu yao pindi wanapokutolea au unapokutana nao ukalazimika kuwatolea salamu, lakini hata hivyo ni wajibu kwako usiwaonyeshe tabasamu.

  • Mhusika: ´Allaamah Ahmad bin Yahyaa an-Najmiy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: http://www.alnajmi.net/voices-action-show-id-118.htm
  • Imechapishwa: 02/12/2018