Swali: Ni ipi ngazi ya Hadiyth hii:

“Hakuna swalah baada ya ´Aswr mpaka lizame jua na wala hakuna swalah baada ya Subh mpaka lichomoze jua isipokuwa Makkah, isipokuwa Makkah, isipokuwa Makkah.”

Jibu: Hadiyth hii kwa nyongeza hii “isipokuwa Makkah” ni dhaifu. Kuhusu msingi wa Hadiyth ni yenye kuthibiti katika “as-Swahiyh” mbili na nyenginezo kutoka kwa kikosi cha Maswahabah (Radhiya Allaahu ´anhum) kutoka kwa Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) ya kwamba amesema:

“Hakuna swalah baada ya Subh mpaka lichomoze jua na wala hakuna swalah baada ya ´Aswr mpaka lizame jua.”[1]

Lakini ueneaji huu ni wenye kuvuliwa zile swalah zenye sababu kwa mujibu wa maoni sahihi zaidi ya wanazuoni. Mfano wa swalah hizo ni kama swalah ya kupatwa kwa jua, swalah ya Twawaaf na swalah ya mamkuzi ya msikiti. Hakika swalah hizi imesuniwa kuziswali ijapo ni wakati wa makatazo kutokana na Hadiyth Swahiyh zilizopokelewa juu yake zinazojulisha juu ya kubaguliwa kwazo kutoka katika ueneaji.

[1] al-Bukhaariy (551) na tamko ni lake, na Muslim (1368).

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Majmuu´-ul-Fataawaa (11/292)
  • Imechapishwa: 03/11/2021