Hakuna siku maalum ya kuyatembelea makaburi

Swali: Ni jambo lina ubaya kufanya matembezi ya kuyatembelea makaburi ni maalum siku ya ijumaa au masiku ya ´Iyd?

Jibu: Haijuzu kuyafanya kuyatembelea makaburi ni jambo maalum siku ya ijumaa au siku ya ´Iyd. Makaburi yanaweza kutembelewa masiku yote. Kusifanywe maalum siku yoyote pasi na dalili. Hakuna dalili iliyopokelewa kwamba makaburi yanatembelewa siku ya ijumaa pekee. Kadhalika masiku mengine. Hakuna dalili ya hilo.

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh Ighaathat-il-Lahfaan (88) https://www.alfawzan.af.org.sa/sites/default/files/igahssat.mp3
  • Imechapishwa: 07/09/2018