Hakuna muda uliopangwa na Shari´ah mume kuwa mbali na mke

Swali: Ni ipi hukumu ya Uislamu juu ya mtu ambaye anamwacha mke wake kwa hoja ya kusafiri kwa ajili ya kazi? Anaweza kuwa mbali naye kwa muda wa mwaka mzima, miaka miwili na wako ambao wanawaacha wake zao kwa muda wa miaka tatu na mke hawezi kumzuia na safari kwa sababu hii ni aibu katika desturi ilioenea. Ni ipi hukumu juu ya haki mke aliyetelekezwa kinyume na ridhaa yake, jambo ambalo linaweza kusababisha mabaya ndani ya jamii. Kwani dini ya mwanamke inapotea bila mchungaji na yeye mwenyewe ndiye anakuwa mchungaji. Ni ipi hukumu ya Shari´ah juu ya hilo? Ni muda kiasi gani mwanamke amsubirie mume wake?

Jibu: Hakuna muda maalum juu ya jambo hili. Lakini ni lazima kwa mume kumcha Allaah juu ya mke wake na wala asiwe mbali naye kwa muda mrefu ambao kunakhofiwa khatari juu yake upande wa mabaya na kuharibika kwa tabia. Anapaswa kumchunga na kumjali. Akiweza kufanya kazi katika mji anaishi [ huyo mke wake] ili awe kwake na alale kwake itakuwa ndio vyema zaidi. Isipomkuia rahisi kwake basi anatakiwa kuzingatia suala la kumtembelea mara kwa mara kwa muda uliokaribu ili asije kutumbukia katika jambo ambalo hautokuwa mzuri mwisho wake.

Imepokelewa kwamba ´Umar (Radhiya Allaahu ´anh) aliwapangia wanajeshi muda wa miezi sita. Hii ni Ijtihaad yake. Wanachuoni wamesema kuwa hili linatofautiana. Miezi sita unaweza kuwa muda wa sawa na mwanamke anaweza kukhofiwa juu yake kwa muda chini ya hapo.

Kwa hiyo mume anatakiwa kuchunga hali ya mke wake, hali ya mji alipo na wale watu waliomzunguka. Anapaswa kuchunga usalama na amani yake. Ikiwa miezi sita ni mingi kwake na ni khatari basi anatakiwa apunguze. Amwendee mara kwa mara kama kila mwezi mmoja au miezi miwili au chini ya hapo. Vovyote atavyoweza kuwa karibu naye ndio wajibu na khaswakhaswa katika zama za khatari kama mfano wa wakati huu. Kwani shari imekithiri, amani imekuwa chache katika miji mingi na machafu yamekuwa mengi. Khaswakhaswa mwanamke akiwa anaishi peke yake basi khatari juu yake ni kubwa. Akiwa anaishi na familia yake waaminifu jambo khatari yake inakuwa ndogo na anasalimika zaidi.

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/6801/%D8%A7%D9%84%D8%AD%D8%AF-%D8%A7%D9%84%D8%B0%D9%8A-%D9%8A%D8%BA%D9%8A%D8%A8-%D9%85%D9%86%D9%87-%D8%A7%D9%84%D8%B1%D8%AC%D9%84-%D8%B9%D9%86-%D8%B2%D9%88%D8%AC%D8%AA%D9%87
  • Imechapishwa: 23/06/2019