Swali: Mwenye kujuzisha mwanamke kuonesha uso na kusema: “Imekatazwa tu pale ambapo kutakhofiwa fitina.” Ni ipi mipaka ya fitina hii?

Jibu: Hili ndilo wanalotakiwa kuulizwa wao. Wanasema kuwa inajuzu kuonesha uso isipokuwa tu pale ambapo kutakhofiwa fitina, waulizwe ni mpaka upi ambao fitina inaaminiwa na mpaka ambao fitina haiwezi kuaminiwa? Hakuna mpaka. Fitina ipo na mwanamke ni fitina na ni ´Awrah vovyote atavyokuwa. Hata akiwa ameshakuwa mtu mzima hata akiwa ni mbaya na si mzuri. Hivyo, wao wenyewe wanakubali kwamba lengo la Hijaab ni kwa ajili ya kuondosha fitina, na fitina sio yenye kuaminika. Hivyo Hijaab (kufunika uso na vitanga) itakuwa ni wajibu.

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: http://www.alfawzan.af.org.sa/ar/node/3234
  • Imechapishwa: 07/02/2018