Swali: Unawanasihi nini makhatwiyb walioko al-Madiynah?

Jibu: Ni jambo lisilokuwa na shaka kwamba makhatwiyb wana majukumu. Wao ndio wanawaelekeza watu katika Khutbah na wanasimama mbele yao katika kila ijumaa. Kwa hivyo wanatakiwa kuiandaa Khutbah vizuri na wazugumze kwa kiasi cha haja ya nchi. Waziwazungumzie watu khabari za ulimwengu na wakatoka pale bila ya faida. Tilia nguvu katika uhalisia wao, yale wanayohitajia na yale makosa wanayofanya. Kwa sababu Khutbah imewekwa katika Shari´ah kwa sababu hii.

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: al-Liqaa’ al-Maftuuh fiy Masjid Qubaa’ http://alfawzan.af.org.sa/ar/node/17626
  • Imechapishwa: 20/02/2018