Hakuna katika Hadiyth Swahiyh jambo la kunyanyua mikono baada ya swalah tano

Swali: Ni ipi hukumu ya kuomba du´aa baada ya swalah na kufuta uso kwa mikono miwili baada ya kumaliza kuomba du´aa?

Jibu: Wanachuoni wamesema kuwa ni Bid´ah kunyanyua mikono baada ya swalah za faradhi. Lakini hata hivyo ni sawa mtu akaomba du´aa baina yake yeye na nafsi yake pasi na kunyanyua mikono.

Ama kuhusu kunyanyua mikono ni jambo limekuja katika Hadiyth ambazo ni dhaifu. Hakuna katika Hadiyth Swahiyh jambo la kunyanyua mikono juu.

  • Mhusika: ´Allaamah ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah ar-Raajihiy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Fataawaa Mutanawwi´ah (05) http://audio.islamweb.net/audio/index.php?page=FullContent&audioid=191110#219240
  • Imechapishwa: 28/10/2018