Hakuna fatwa inayokubalika isipokuwa kwa dalili


Swali: Kuna ambao wanasherehekea sherehe za kuzaliwa kwa watoto wao na wanatumia hoja kwa Fatwa ya mlinganizi mmoja ambaye anajulikana. Je, dhimma yao inatakasika kwa kuamini hivi?

Jibu: Fatwa haikubaliki isipokuwa kwa dalili. Iko wapi dalili ya aliyejibu hivi ya kwamba inajuzu kusherehekea kuzaliwa kwa mvulana au msichana? Dalili iko wapi? Hakuna dalili juu ya Fatwa hii.

Linalomlazimu ni yeye kumshukuru Allaah kwa kupata mtoto. Kadhalika afanye Sunnah kwa mtoto huyu:

1- Amfanyie ´Aqiyqah kwa kumchinjia mvulana mbuzi mbili na msichana mbuzi mmoja.

2- Amchagulie jina zuri.

3- Amtahiri. Kutahiri ni katika Sunnah ya Mitume (´alayhimus-Swalaatu was-Salaam).

Anatakiwa vilevile kumsomea Ruqyah, kumwamrisha swalah atapofikisha miaka saba na kumpiga kwayo anapofikisha miaka kumi.

Kuhusiana na sherehe hizi ni kitu kisichokuwa na asli. Jengine ni kwamba hakuna mwenye kufaidika nazo; si mzazi wala mtoto.

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Duruus-ul-Haram http://www.alfawzan.af.org.sa/node/13974
  • Imechapishwa: 16/04/2018