Swalah ina sifa nyingi za kipekee ikiwa ni pamoja na:

1- Swalah ndio yenye kupambanua kati ya muislamu na kafiri.

2- Swalah ndio kitendo cha kwanza ambacho mja atahesabiwa akiwa ndani ya kaburi.

3- Swalah ndio ´ibaadah bora na tukufu zaidi.

Yule ambaye haswali amekata mahusiano kati yake yeye na Allaah. Swalah ndio mafungamano na mahusiano kati yako wewe na Allaah. Hivyo ni lazima kwa muislamu atilie umuhimu kwelikweli jambo la swalah. Ni lazima aziswali swalah ndani ya wakati wake. Pambana na nafsi yako. Weka alamu kwenye saa, simu yako au muombe mtu akuamshe wakati wa swalah kama Fajr, ´Aswr na swalah zengine. Jambo ni la khatari sana. Mtu kufunga na kupuuzilia mbali swalah ni kwamba anahifadhi nguzo ya nne ya Uislamu na anapuuza nguzo ya pili ya Uislamu? Faida iko wapi? Ambaye anafunga lakini haswali hafaidiki kitu. Swawm haisihi isipokuwa pamoja na swalah. Akiacha swalah swawm yake haisihi. Kuacha swalah ni ukafiri na kuritadi kutoka katika Uislamu. Mtu akiacha swalah basi swawm, hajj na matendo yake mengine yote hayasihi.

  • Mhusika: ´Allaamah ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah ar-Raajihiy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: http://shrajhi.com.sa/uploads/rmadhan_02.mp3
  • Imechapishwa: 08/05/2019