Swali: Ni ipi du´aa iliopokelewa kutoka kwa Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) wakati wa kukata swawm na wakati wa kula daku?

Jibu: Imepokelewa kutoka kwa Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) ya kwamba alikuwa akisema wakati wa kukata swawm:

ذَهَبَ الظَّمَأُ وَابْتَلَّتِ الْعُرُوقُ وَثَبَتَ الْأَجْرُ إِنْ شَاءَ اللَّهُ

“Kiu kimeondoka, mishipa imerowana na ujira umepatikana – Allaah akitaka.”[1]

Vilevile imepokelewa kutoka kwa baadhi ya Maswahabah kwamba walikuwa wakisema wakati wa kukata swawm:

اللهم لك صمت وعلى رزقك أفطرت فاغفر لي إنك أنت الغفور الرحيم

“Ee Allaah! Nimefunga kwa ajili yako na nimefutari kwa riziki yako. Kwa hiyo nisamehe, kwani hakika Wewe ni Mwingi wa kusamehe, Mwenye kurehemu.”[2]

Kuhusu daku, kutokana na ninavojua hakukupokelewa du´aa maalum inayosemwa wakati wa kufanya hivo.

[1] Abu Daawuud (2357), al-Bayhaqiy katika ”as-Sunan al-Kubraa” (4/239) na katika ”as-Sunan as-Sughraa” (1390) na ad-Daaraqutwniy (240). Nzuri kwa mujibu wa al-Albaaniy katika ”Irwaa’-ul-Ghaliyl”.

[2] Abu Daawuud (2358), ad-Daaraqutwniy (240) na Ibn-us-Sunniy katika ”´Amal-ul-Yawm wal-Laylah” (482). Ibn-ul-Qayyim amesema:

”Haikuthibiti.” (Zaad-ul-Ma´aad (2/51))

Ibn Hajar amesema:

”Cheni ya wapokezi ni dhaifu.” (Talkhiysw-ul-Habiyr)

Dhaifu kwa mujibu wa al-Albaaniy katika ”Dhwa´iyf Sunan al-Albaaniy” (2358).

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Majmuu´-ul-Fataawaa (02/395)
  • Imechapishwa: 26/03/2022