Swali: Ni zipi nasaha zako juu ya mapote ya wapinzani ambayo yanawachukia Ahl-us-Sunnah wal-Jamaa´ah? Ni lipi kundi lililookoka? Ni ipi hukumu ya wale wanaowachukia Maswahabah wa Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam)?

Jibu: Kundi lililookoka limebainishwa na Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) pale aliposema:

“Ni lile litalokuwa juu ya yale niliyomo mimi hii leo na Maswahabah wangu.”

Hili ndio kundi lililookoka:

Ni wale waliyomo juu ya yale aliyomo Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) na Maswahabah wake; juu ya Qur-aan, Sunnah na yale waliyokuwemo Salaf wa Ummah huu. Hawa ndio kundi lililookoka.

Kuhusu kuwachukia Ahl-us-Sunnah wal-Jamaa´ah au kuwachukia Maswahabah ni unafiki. Huu ni unafiki na ulinzi unatakwa kutoka kwa Allaah. Hakuna anayewachukia Maswahabah isipokuwa mnafiki. Hakuna anayewachukia Ahl-us-Sunnah wal-Jamaa´ah isipokuwa mnafiki tu. Allaah (Jalla wa ´Alaa) pindi alipowataja Maswahabah mwishoni mwa Suurah “al-Fath” akasema:

لِيَغِيظَ بِهِمُ الْكُفَّارَ

“… ili liwaghadhibishe makafiri.” (48:29)

Hakuna yeyote anayemtukana Swahabah wa Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) isipokuwa tu kafiri au mnafiki ambaye unafiki wake unajulikana.

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: https://www.youtube.com/watch?v=oMoaMLGx4k0
  • Imechapishwa: 26/11/2017