Hakuna anayefanya ushabiki isipokuwa mpumbavu au mwendawazimu

Swali: Tunataraji utatubainishia ukhatari wa kuwa na ushabiki. Wapo baadhi ya vijana ambao wana ushabiki kwa baadhi ya watu kwa njia ya kwamba wako tayari kupenda na kujenga uadui kwa ajili yao. Tunaomba utupe maneno ya mwongozo kwani huenda Allaah akatunufaisha kwayo.

Jibu: Ushabiki ni jambo lenye kusemwa vibaya. Bali ni katika mifuno ya makafiri. Ushabiki na kufuata matamanio ni katika njia za watu wa kipindi cha kikafiri. Vilevile ni katika njia za watu wa Tatari, kama anavosema Shaykh-ul-Islaam Ibn Taymiyyah.

Muumini anatakiwa kujitahidi kuitambua haki na kushikamana nayo japokuwa haki hii itamkhalifu mwenye kuikhalifu. Asiwe na ushabiki hata siku moja juu ya kosa au maoni ya fulani. Anachotakiwa ni kushikamana barabara na Qur-aan na Sunnah. Awe tayari kupenda na kujenga uadui kwa mujibu wa yale aliyokuja nayo Muhammad (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) baada ya kuyajua fika. Haitakiwi iwe mambo ya kudhania. Iwe baada ya kujua kwamba jambo fulani limekuja na Muhammad (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam), limefahamishwa na Qur-aan na Sunnah na Salaf wakalichukulia dini.

Ibn-ul-Qayyim anaona kuwa utapolijua andiko na ukalifahamu, kwa msemo mwingine hata kama hukujua yule aliyelisema, basi ni lazima kwako kushikamana nalo. Pindi utapowajua wale waliolitamka basi hilo likuzidishie nguvu na yakini zaidi. Si sharti awepo mtu aliyelitamka. Muhimu ni kwamba anachotakiwa muislamu kukitilia manani ni yale yaliyosemwa na Allaah na Mtume Wake. Ama aje mtu mjinga na kujifanya mwenyewe ameshakuwa imamu na akaingia katika mambo ya batili na wewe ukafanya ushabiki kwake, haya ni miongoni mwa matendo ya kipindi cha kikafiri. Bali hata akiwa ni imamu kweli ambapo akakosea na wewe ukafanya ushabiki kwake, basi wewe una chembechembe za kipindi cha kikafiri:

إِنَّا وَجَدْنَا آبَاءَنَا عَلَىٰ أُمَّةٍ وَإِنَّا عَلَىٰ آثَارِهِم مُّهْتَدُونَ

“Hakika sisi tumewakuta baba zetu juu ya dini na hakika sisi tunajiongoza kwa kufuata athari zao.” (43:22)

Ushabiki huu ni miongoni mwa mambo na matendo ya watu wa kipindi cha kikafiri. Ama kuhusu muislamu wa haki ni lazima kwake kujitakasa na ushabiki na kwenda kinyume na yale aliyokuja nayo Muhammad (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam). Ushabiki ni jambo baya. Hakuna anayefanya ushabiki isipokuwa shabiki au mtu mwenye kusemwa vibaya.

Shabiki ni mwendawazimu ambaye amepatwa na maradhi ya ushabiki na mpumbavu (غبي). Hakuna anayefanya ushabiki isipokuwa mpumbavu au shabiki. Muislamu anatakiwa kujitakasa na asiwe mpumbavu, mwendawazimu wala shabiki. Anatakiwa awe mwenye busara ambaye anatafuta haki. Akiijua haki basi aifuate japokuwa itakuwa ni yenye kwenda kinyume na wale wote waliyomo ardhini. Asiwe na ushabiki kwa imamu, maamuma, mkweli wala muongo. Shani ya mambo ni kwamba anatakiwia kushikamana na haki.

  • Mhusika: ´Allaamah Rabiy´ bin Haadiy al-Madkhaliy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: https://www.sahab.net/forums/index.php?app=forums&module=forums&controller=topic&id=163317
  • Imechapishwa: 01/09/2018