Imaam at-Twahaawiy (Rahimahu Allaah):

“Hakukuwi isipokuwa yale Anayoyataka.”

Hapa kuna uthibitisho wa Sifa ya matakwa. Kila kinachokuwa kwenye ulimwengu huu basi Allaah Amekitaka. Hakupitiki kwenye ufalme wa Allaah isipokuwa yale Anayoyataka. Kwa kuwa Allaah Yeye ndiye Mfalme na Mwendeshaji. Hakukiwi kwenye ufalme Wake isipokuwa kile Anachokitaka kati ya dhati, sifa na matendo.

at-Twahaawiy (Rahimahu Allaah) amechokusudia ni kutaka kuwaraddi Qadariyyah katika Mu´tazilah ambao wanasema kuwa kunaweza kupitika kwenye ufalme wa Allaah kitu asichokitaka. Wanasema kuwa Allaah (Ta´ala) ametaka watu wote wawe na imani, lakini hata hivyo kafiri na mtenda maasi wametaka kufuru na maasi na hivyo ndio kukawa kumetokea kufuru ilihali Allaah haitaki kufuru kama jinsi wametumbukia kwenye maasi ilihali Allaah hataki maasi. Wakawalazimisha Ahl-us-Sunnah wal-Jamaa´ah juu ya kwamba kunapatika kwenye ufalme wa Allaah kile asichokitaka. Hili linalazimisha kumtia mapungufu Allaah (´Azza wa Jall).

Ahl-us-Sunnah wal-Jamaa´ah wanasema kuwa Allaah (Ta´ala), hata kama ametaka kupitike kufuru na maasi kilimwengu na kimakadirio, lakini hata hivyo hayapendi kidini na Kishari´ah, hayaridhii na hayaamrishi. Bali kinyume chake anayakataza na kuyachukia.

  • Mhusika: ´Allaamah ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah ar-Raajhiy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: al-Hidaayah ar-Rabbaaniyyah fiy Sharh al-´Aqiydah at-Twahaawiyyah (01/55)
  • Imechapishwa: 07/06/2020