Hakuhitajiki nia ili kuondosha najisi

Swali: Ni lazima ninuie kuondosha najisi kutoka kwenye tupu ya mbele na ya nyuma ili niweze kutawadha?

Jibu: Hakuhitajiki nia ili kuondosha najisi zote. Kwa sababu najisi ni katika mambo ya kuacha. Najisi ikiondoka yenyewe au ikitoka kwa kitu kingine kuiondosha, inatosha. Kwa mfano kama juu ya ardhi kuna najisi na mto ukapita juu yake na kuiondosha, sehemu hiyo ya ardhi inakuwa safi hata kama wewe hukuisafisha wala hukunuia hilo. Mto umeitwahirisha. Kuondoka kwa najisi hiyo ardhi hiyo imekuwa safi. Bali wanachuoni wamesema hata myale ya jua inasafisha ikiwa najisi hiyo na harufu yake inaondoka. Hata upepo unaweza pia kusafisha.

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh Ighaathat-il-Lahfaan (42) http://alfawzan.af.org.sa/sites/default/files/ighastah%20%20-%2011%20-%201%20-%201437.mp3
  • Imechapishwa: 14/03/2017