“Hakika Allaah yupamoja na wale wenye kusubiri”


Swali: Kunapokimiwa swalah basi baadhi ya watu ambao wamechelewa wanakuja hali ya kukimbia na kusema:

إِنَّ اللَّهَ مَعَ الصَّابِرِينَ

“Hakika Allaah yupamoja na wale wenye kusubiri.”

Ni ipi hukumu ya kukimbia katika swalah?

Jibu: Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:

“Mnaposikia Iqaamah basi tembeeni hali ya utulivu. Kile mtachowahi swalini. Kile kitachowapiteni kitimizeni.”

Katika upokezi wingine:

“Kikidhini.”

Huu ndio mwongozo wa Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam).

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: http://alfawzan.af.org.sa/ar/node/16832
  • Imechapishwa: 17/03/2018