Swali: Ni ipi dalili ya Kishari´ah juu ya kupatikana kwa idhini ya mtawala au wazazi wawili kwa ajili ya kupigana Jihaad katika njia ya Allaah?

Jibu: Kauli ya Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) juu ya yule aliyekuja na kutaka kwenda katika Jihaad pamoja na Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) na akamwambia:

“Je, wazazi wako wako hai?”

Akasema:

“Ndio.”

Akamwambia:

“Kapigne nao Jihaad.”

Isitoshe, Allaah Amefanya haki ya wazazi wawili kuwa baada Yake (Subhaanahu wa Ta´ala). Haki ya wazazi wawili ni wajibu wakati Jihaad kwa njia ya kijumla ni Sunnah. Isipokuwa katika hali ambazo wanachuoni wamesema kuwa inakuwa faradhi kwa watu wote [ndio hakuhitajiki idhini ya wazazi]. Jihaad nje ya hali hizi tatu, inakuwa ni Sunnah iliyokokotezwa. Wajibu ni wenye kutangulizwa kabla ya Sunnah.

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh ´Aqiydat-is-Saffaariniyyah (14) http://www.alfawzan.af.org.sa/sites/default/files/sfranih_14.mp3
  • Imechapishwa: 19/06/2018