Haki itabainishwa aridhie mwenye kuridhia na kukasirika mwenye kukasirika


Swali: Ni ipi hukumu ya ambaye anatetea vitabu vya Ahl-ul-Bid´ah na Ahl-ut-Takfiyr na anawashauri vijana kuvisoma na anawakemea wale wanaovitahadharisha?

Jibu: Huyu ni mwenye kuufanyia ghushi Ummah. Ambaye anasisitiza kusoma vitabu vya upotevu na vitabu vya utata anaufanyia ghushi Ummah. Vilevile anaifanyia ghushi Qur-aan na Sunanh:

“Dini ni kupeana nasaha.” Tukasema: “Kwa nani?” Akasema: “Kwa Allaah, Kitabu Chake, Mtume Wake na viongozi wa waislamu na watu wa kawaida.”

Ni lazima kubainisha haki. Ni lazima kuweka haki wazi. Ni lazima kulingania katika haki. Lazima haya yafanyike na aridhie yule mwenye kuridhia na akasirike yule mwenye kukasirika.

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: http://alfawzan.af.org.sa/ar/node/17750
  • Imechapishwa: 11/04/2018