Hajj za wazazi wawili zinamuwajibikia nani?

Swali: Ni nani ambaye ana jukumu la kumuhijia baba na mama wakiwepo lakini wasiwe na uwezo wa kuhiji?

Jibu: Hakuna mtu yeyote ambaye amekalishwa juu yao. ´Ibaadah zinamuwajibikia ambaye amekalifishwa na si mwengineo. Lau ´ibaadah ya mtu ingekuwa ni yenye kumuwajibikia mwengine basi ingelipelekea kupata dhambi kwa kule kuipoteza. Amesema (Ta´ala):

وَلَا تَزِرُ وَازِرَةٌ وِزْرَ أُخْرَىٰ

“Wala habebi mbebaji mzigo [wa dhambi] wa mtu mwengine.”[1]

Wazazi wawili wakiwa hawawezi kuhiji kwa miili yao pamoja na kwamba pesa zipo, basi wanatakiwa kufanyiwa hajj na mmoja katika watoto. Ikiwa wanaweza kuhiji kwa miili yao basi haijuzu kwa yeyote kuwahijia ile hajj ya kwanza ambayo ni nguzo ya Uislamu. Ama mbali na hiyo hakuna neno kufanya hivo.

[1] 06:164

  • Mhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Nuur ´alaad-Darb (06) http://binothaimeen.net/content/6687
  • Imechapishwa: 28/11/2020