Swali: Je, hajj ya mtu ambaye amehiji kwa mali ambayo baadhi yake inatokana na ribaa inasihi? Ni kipi kinachomlazimu?

Jibu: Ni lazima kwake kutubia na kujutia. Akihiji kwa pesa ya haramu basi hapati thawabu. Hata hivyo hajj yake ni sahihi. Imesemekana:

Ukihiji kwa pesa inayotokana na pesa ya haramu, basi hukuhiji bali ni aibu tupu

Kwani Allaah hakubali isipokuwa chumo lililo zuri

Si kila anayehiji katika Nyumba ya Allaah hajj yake ni yenye kukubaliwa.

Huyu ni kama mfano wa ambaye amemwendea kuhani na akamsadikisha, basi hazitokubaliwa swalah zake kwa siku arubaini. Hiyo ina maana kwamba hatolipwa thawabu kwa swalah zake lakini hata hivyo ni zenye kusihi.

  • Mhusika: ´Allaamah ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah ar-Raajihiy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Fataawaa Mutanawwi´ah (18)
  • Imechapishwa: 23/01/2021