Hajj ya mwenye kurudi kuswali baada ya kuacha

Swali: Mwenye kuhiji na wakati huo alikuwa anaswali. Kisha baada ya hapo akapinda na kuacha swalah. Kisha akatubu na kurudi kuanza tena kusimamisha swalah. Je, Hajj yake ya kwanza inazingatiwa kuwa ni Hajj ya Uislamu?

Jibu: Lililo salama zaidi ni yeye kurudi kuhiji tena. Kuna tofauti juu ya kwamba akitubu kwa Allaah matendo yake aliyofanya kabla ya kuritadi yanamrudilia au hayamrudilii na badala yake yanaharibika? Kuna tofauti kwa wanachuoni. Lililo salama zaidi ni yeye kurudi kuhiji tena ili aitakase dhimma yake kwa yakini.

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: at-Tafsiyr al-Mufasswal (26) http://www.alfawzan.af.org.sa/sites/default/files/tf–1428-4-6.mp3
  • Imechapishwa: 19/08/2020