Swali: Kijana akiwa ni muweza wa kuhiji ambapo akachelewesha mpaka pale atakapooa au akawa mkubwa kiumri – je, anapata dhambi?

Jibu: Akibaleghe na yeye ni muweza wa kuhiji na kufanya ´Umrah, basi ni wajibu kwake kuyatekeleza. Hayo ni kutokana na ueneaji wa dalili ikiwa maneno Yake (Subhaanah):

وَلِلَّـهِ عَلَى النَّاسِ حِجُّ الْبَيْتِ مَنِ اسْتَطَاعَ إِلَيْهِ سَبِيلًا

“Kwa ajili ya Allaah imewawajibikia watu watekeleze Hajj katika Nyumba hiyo kwa mwenye uwezo.” (03:97)

Lakini yule mwenye haja ya kuoa basi ni wajibu kwake kuharakisha kuoa kabla ya kuhiji. Kwa sababu katika hali hii haitwi kuwa ni mwenye uwezo. Ikiwa hawezi kujihudumia jambo la kuoa na kuhiji kwa wakati mmoja, basi aanze kwanza kuoa ili aihifadhi nafsi yake. Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:

“Enyi kongamano la vijana! Yule ambaye katika nyinyi ana uwezo wa kuoa basi na aoe. Kwani jambo hilo linamfanya kuteremsha macho na kumlindia tupu yake. Na yule asiyeweza basi na afunge – kwani hiyo ni ngao kwake.”

Ameipokea al-Bukhaariy na Muslim.

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Min as-ilah Duruus Buluugh-il-Maraam
  • Imechapishwa: 15/03/2019