Miongoni mwa mambo yanayomzuia mtu na elimu ni kule kuchukua kwake elimu kutoka kwa wadogo. Miongoni mwa alama za Qiyaamah ni kule elimu kuchukuliwa kutoka kwa wadogo na vijana. Wanajifunza elimu kidogo na tahamaki anajiona kuwa ni mwanachuoni. Mtu [daima] ni mdogo na masikini. Lakini hata hivyo tahamaki anajiona amefika ukomo, anajitokeza, anajiwa na ujinga, wanamzunguka pambizoni mwake na anawatenga wanachuoni wengine. Hii ni alama ya Qiyaamah. Miongoni mwa alama ni watu kuwaacha wanachuoni wakubwa na badala yake wakaenda kuchukua elimu kutoka kwa wajinga, wadogo na wenye kujifanya ni wanachuoni. Hii ni balaa.

  • Mhusika: ´Allaamah Rabiy´ bin Haadiy al-Madkhaliy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Marhaban yaa Twaalib-il-´Ilm, uk. 228
  • Imechapishwa: 10/03/2018