Haiwezekani kuthibitisha imani ya ´Aliy bila ya kuthibitisha ya Abu Bakr na ´Umar

Wakitaka kuthibitisha imani na uadilifu wa ´Aliy kwa Qur-aan, basi wataambiwa kuwa Qur-aan imekuja kwa jumla. Qur-aan kumrejea yeye sio vikubwa kuliko inavyowarejea wengine. Hakuna Aayah hata moja wanayosema kuwa ni maalum kwake isipokuwa Aayah hiyohiyo, au mfano wake au kubwa kuliko hiyo, ni maalum kwa Abu Bakr na ´Umar. Siku zote ni rahisi kudai pasi na dalili wala hoja. Ni rahisi kudai fadhilah juu ya Abu Bakr na ´Umar kuliko mwingine yeyote wasiokuwa wao.

Wakisema kuwa hayo yamethibiti kwa nukuu na mapokezi, nasi nukuu na mapokezi kwa wale wengine ni yenye kutambulika vyema na mengi zaidi.

Wakisema kwamba imepokelewa kwa njia nyingi, basi mapokezi kwa njia nyingi kwa wale wengine ni sahihi zaidi.

Kama wanategemea nukuu za Maswahabah, basi nukuu za Maswahabah kwa wale wengine ni nyingi zaidi.

Aidha wanasema kuwa Maswahabah waliritadi isipokuwa watu wachache tu. Ni vipi basi mtu atayakubali mapokezi ya watu hawa juu ya fadhilah za mtu? Wala kati ya Maswahabah hapakuwa Raafidhwah wengi mpaka waweze kupokea fadhilah hizi kwa njia nyingi. Hawawezi kupokea kitu midhali hawataki kufuata njia ya Ahl-us-Sunnah kama ambavyo manaswara hawawezi kuthibitisha utume wa ´Iysaa wasipofuata dini ya waislamu.

Kwa hivyo Raafidhwah ni watu walio wajinga na wapotevu kabisa kama ambavyo manaswara ndio wapotevu zaidi. Kadhalika Raafidhwah ndio watu wachafu zaidi kama ambavyo mayahudi ni watu wachafu zaidi. Wana aina fulani ya upotevu wa manaswara na uchafu wa mayahudi.

  • Mhusika: Shaykh-ul-Islam Ahmad bin Taymiyyah
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Minhaaj-us-Sunnah an-Nabawiyyah (2/63-64)
  • Imechapishwa: 10/12/2018