Hata wale watu wenye dini wanapoketi mahali fulani pengine wakasengenya. Huenda wakati mwingine usengenyi wa watu wa dini unaweza kuwa khatari na kubwa zaidi. Wanaweza kuwasengenya wanachuoni, walinganizi, viongozi na watawala. Kuwasengenya watu hawa na wengineo wenye mamlaka, ingawa ni wenye mamlaka ya ngazi ya chini kama mfano wa mudiri wa masomo, ni jambo la khatari zaidi kuliko kumsengenya mtu wa kawaida.

Kwa mfano tukiwasengenya wanachuoni, basi umainifu wa watu juu yao unapotea. Ikiwa uaminifu wa watu juu yao utapotea basi inakuwa ni vigumu kwa watu kukubali yale wanayoyasema katika Shari´ah ya Allaah. Jambo hili lina khatari kubwa.

Tukiwasengenya viongozi au watawala, basi inapungua heshima ya watu juu yao na inakuwa ni rahisi kwao kuwaasi. Ni jambo lina athari kubwa katika amani. Kwa hiyo ikawa jambo la kuwasengenya wanachuoni na viongozi ni kubwa zaidi kuliko watu wa kawaida. Kwa sababu kuwasengenya watu wa kawaida ni jambo limefupika mtu kwa dhati yake mwenyewe kwa vile hana uongozi wowote katika jamii.

  • Mhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Liqaa’ al-Baab al-Maftuuh (30 A)
  • Imechapishwa: 13/09/2020