Haitakiwi kutembea na viatu makaburini

Swali: Ni ipi hukumu ya kupita kati ya makaburi kwa viatu?

Jibu: Heshima ya maiti ni kama heshima yake alipohai. Haitakiwi kwa mtu achukue wepesi suala hili. Haitakiwi kwa mtu kutembea kwa viatu vyake isipokuwa wakati wa haja. Kwa mfano ardhi ina joto kali, ngumu sana, ina miba au changarawe.

  • Mhusika: ´Allaamah ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah ar-Raajihiy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Fataawaa Mutanawwi´ah (15)
  • Imechapishwa: 20/06/2020