Hairuhusu kumuoa malaya


Swali: Nini maana ya neno Lake (´Azza wa Jall):

الزَّانِي لَا يَنكِحُ إِلَّا زَانِيَةً أَوْ مُشْرِكَةً

“Mwanamme mzinifu haowi isipokuwa mwanamke mzinifu au mwanamke mshirikina.” (24:03)

Je, ina maana ya kwamba imeruhusiwa kwake jambo hili?

Jibu: Hapana. Haina maana kwamba amepewa idhini ya kufanya hivo. Hapa kunaenezwa hali ilivyo kwa lengo la kumzuia. Sio kwa lengo la kuruhusu ya kwamba imeruhusiwa kwake kumuoa mzinifu.

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh Ighaathat-il-Lahfaan (67) http://alfawzan.af.org.sa/sites/default/files/Ighastah22-05-1438h.mp3
  • Imechapishwa: 18/10/2017