Hairuhusu kufupisha swalah ukishafika katika mji wako

Swali:  Nilikuwa nimesafiri nje ya nchi yetu kisha nikarudi baada ya siku chache. Nilipoingia katika nchi yangu ulikuwa umeingia wakati wa ´Ishaa. Baadhi ya ndugu wakanifutu kwamba niswali kwa kufupisha. Je, ni wajibu kwangu kuirudi swalah hii ilihali kumeshapita miaka miwili?

Jibu: Ndio, swalah yako ni batili. Ukifika katika nchi yako huruhusiwi kufupisha. Hukumu za safari zimekwisha na unatakiwa kuswali Rak´ah nne. Haijalishi kitu hata kama kumekwishapita miaka mia moja hivi sasa unatakiwa kulipa Rak´ah nne.

  • Mhusika: ´Allaamah ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah ar-Raajihiy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Fataawaa Mutanawwi´ah (05) http://audio.islamweb.net/audio/index.php?page=FullContent&audioid=191110#219240
  • Imechapishwa: 05/10/2018