Swali: Imekuwa ni jambo la kawaida katika baadhi ya nchi za Kiislamu mwanamke anachukua jina la mume wake au jina lake la utani. Kwa mfano mwanamke anaitwa Zaynab ambaye ameolewa na Zayd anabadili jina lake la ubini Zaynab Zayd au ni katika desturi ya kimagharibi ambayo ni lazima kujiepusha nayo?

Jibu: Haijuzu kwa mtu kujinasibisha kwa mtu mwingine asiyekuwa baba yake. Allaah (Ta´ala) amesema:

ادْعُوهُمْ لِآبَائِهِمْ هُوَ أَقْسَطُ عِندَ اللَّهِ

“Waiteni kwa baba zao, maana huo ndio uadilifu zaidi mbele ya Allaah.” (33:05)

Kumetajwa matishio makali kwa yule mwenye kujinasibisha kwa mtu mwingine asiyekuwa baba yake.

Kutokana na haya haijuzu kwa mwanamke kujinasibisha kwa mume wake, jambo ambalo linafanywa na makafiri na waislamu ambao wanajifananisha nao.

  • Mhusika: al-Lajnah ad-Daaimah
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: al-Fataawaa al-Qayyimah lil-Usrah al-Muslimah, uk. 70
  • Imechapishwa: 12/09/2020
  • mkusanyaji: Sa´d ´Abdul-Ghaffaar ´Aliy