Haijuzu kuweka kikomo katika uzazi

Swali: Kuweka kikomo cha uzazi au kama wanavosema uzazi wa mpango kwa dharurah kama mfano wa kuhifadhi afya ya mama au kutilia umuhimu malezi ya watoto – je, ni kitendo cha halali au cha haramu? Hili khasa pale ambapo mwanamke atakuwa ni mwenye kuzaa sana?

Jibu: Kitendo hichi hakijuzu. Akilazimika basi afanye al-´Azl, bi maana anapotaka kutokwa na manii basi anamwaga nje kwa kuchopoa dhakari yake kutoka kwenye tupu ya mwanamke. Vinginevyo jambo hili la kuweka kikomo cha uzazi na mengineyo Allaah (Subhaanahu wa Ta´ala) amesema:

وَلَا تَقْتُلُوا أَوْلَادَكُم مِّنْ إِمْلَاقٍ ۖ نَّحْنُ نَرْزُقُكُمْ وَإِيَّاهُمْ

“Wala msiwaue watoto wenu kutokana na umasikini – Sisi Tunakuruzukuni pamoja.” (al-An´aam 06:151-152)

Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:

“Oaneni mkithiri. Kwani hakika mimi nitajifakhari kwa ajili yenu nyumati zengine siku ya Qiyaamah.”

Jengine ni kwamba Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) alimuombea Anas bin Maalik awe na mali na kizazi kingi.

  • Mhusika: ´Allaamah Muqbil bin Haadiy al-Waadi´iy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Ijaabatu as-Saa-il, uk. 589
  • Imechapishwa: 24/02/2020