Haijuzu kusherekea kuzaliwa kwa Mtume wala kuzaliwa kwa mwengine yeyote

Swali: Je, imethibiti kwamba Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) alizaliwa tarehe 12 Rabiy´ al-Awwaal? Ni ipi hukumu ya kusherehekea siku ya kuzaliwa kwake?

Jibu: Haijuzu kusherehekea siku ya kuzaliwa kwake. Alizaliwa (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) Rabiy´ al-Awwaal. Lakini haifai kusherehekea siku ya kuzaliwa kwake. Hii ni Bid´ah. Kila Bid´ah ni upotevu. Amesema (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam):

“Tahadharini na mambo yaliyozuliwa. Kwani hakika kilichozuliwa ni Bid´ah, kila Bid´ah ni upotevu na kila Bid´ah ni Motoni.”

Haijuzu kusherekea kuzaliwa kwa Mtume wala kuzaliwa kwa mwengine yeyote.

Usile chakula kilichotengenezwa kwa ajili ya maulidi. Chakula kilichotengenezwa kwa mnasaba wa maulidi usikile.

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh Ighaathat-il-Lahfaan (98) https://www.alfawzan.af.org.sa/ar/node/18006
  • Imechapishwa: 15/05/2019