Haijuzu kurejesha zawadi uliyokwishapeana

Swali: Je, inafaa kwa baba kurejesha kile alichokwishakitoa kumpa mwana wake?

Jibu: Inafaa kufanya hivo akiona kuna manufaa ya kufanya hivo na mtoto akaweza kumrudishia baba yake. Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:

“Si halali kwa mtu muislamu kupeana zawadi kisha akairudisha isipokuwa baba kwa kile anachompa mtoto wake.”

Ameipokea Imaam Ahmad, Abu Daawuud, at-Tirmidhiy, an-Nasaa´iy na Ibn Maajah na ameisahihisha at-Tirmidhiy, Ibn Hibbaan na al-Haakim.

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Majmuu´-ul-Fataawaa (09/300)
  • Imechapishwa: 18/07/2021