Swali: Je, inajuzu kwangu kuoa mwanamke ambaye nilinyonya kwa mama yake lakini yeye hakunyonya kwa mama yangu?

Jibu: Haijuzu kwa kuwa huyo huchukuliwa kuwa ni dada yake katika kunyonya. Na Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) anasema: “Ni Haramu kwa kunyonya kama yalivyo Haramu yanayopatikana katika nasabu.”

  • Mhusika: ´Allaamah Muqbil bin Haadiy al-Waadi´iy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Imechapishwa: 05/03/2018