Haijuzu kunyamazia maovu eti kwa ajili ya kueneza Tawhiyd na Sunnah


Swali: Je, inafaa kwa mtu kutumia fursa ya hali na kulingania katika Tawhiyd, Uislamu au Sunnah pasi na kukemea maovu yanayopatikana mahali hapo?

Jibu: Hapana. Haijuzu. Haijuzu. Hili ndilo nililokuwa nachelea. Ni kwa nini asikusanye kati ya mazuri mawili kwa wakati mmoja? Ni kwa nini asikemee maovu anayoyaona mbele yake na kulingania katika Tawhiyd? Kwa sababu atakuwa amechukulia kule kunyamazia maovu kuwa ni njia ya kulingania katika Tawhiyd. Kwa ajili hiyo tunarejesha njia hizi katika zile njia za mwanzo tulizokuwa tukizungumzia, nazo ni kwamba haijuzu kutumia njia za pumbao kuwa ni njia ya kuwalingania watu katika Uislamu. Kwa ajili hiyo itakuwa ni aula zaidi kutonyamazia maovu yanayotokea mbele yetu kwa ajili ya kukemea maovu makubwa zaidi. Lengo zuri haitakasi njia. Ukiwa mbele ya maovu, basi unalazimika kuyakemea na khaswa ikiwa dalili za maovu haya unazipata kwenye vitabu vya Mashaykh hawa ambao wanawarejelea wazushi hawa.

Kwa hiyo sura hii iliyotajwa katika swali la mwisho haijuzu. Badala yake analazimika kukusanya kati ya kukemea maovu ambayo wao wanatumbukia ndani yake na kuwalingania katika Tawhiyd. Namna hii ndivo anavotakiwa kufanya na Allaah (Ta´ala) ndiye mjuzi zaidi.

  • Mhusika: Imaam Muhammad Naaswir-ud-Diyn al-Albaaniy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Fataawaa Juddah (16 B)
  • Imechapishwa: 31/01/2021