Haijuzu kugusa dhakari kwa mkono

Swali: Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:

“Mmoja wenu asiguse dhakari yake kwa mkono wake wa kuume ilihali anakojoa.”

Je, kugusa dhakari kwa mkono wa kulia ni haramu kwa hali zote au ni wakati wa kutawadha peke yake?

Jibu: Hapana, ni katika hali zote. Lakini hata hivyo wakati wa kukojoa imekatazwa zaidi. Vilevile katika hali isiyokuwa ya kukojoa haijuzu. Akihitajia kuigusa basi aiguse kwa mkono wake wa kushoto.

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh ´Umdat-il-Fiqh (04) http://www.alfawzan.af.org.sa/sites/default/files/omdh–14340323.mp3
  • Imechapishwa: 25/08/2020