Haijuzu kuapa kwa Mtume


Swali: Vipi kuhusu kuapa kwa Mtume (و النبي) ?

Jibu: Hiki ni kiapo. Haijuzu. Haijuzu kuapa isipokuwa kwa jina la Allaah. Amesema (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam):

“Mwenye kuapa basi aape kwa Allaah au anyamaze.”

“Mwenye kuapa kwa asiyekuwa Allaah amekufuru au kushirikisha.”

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: al-Liqaa' al-Maftuuh fiy Masjid Qubaa' http://alfawzan.af.org.sa/ar/node/17626
  • Imechapishwa: 24/02/2018