Haijuzu kuandika chochote juu ya kaburi

Swali: Je, inafaa kuweka kipande cha chuma au ishara juu ya kaburi la maiti iliyoandikwa Aayah ya Qur-aan na kuongezea jina la maiti na tarehe ya kufariki kwake?

Jibu: Haijuzu kuandika juu ya kaburi la maiti si Aayah ya Qur-aan wala kitu kingine. Ni mamoja juu ya chuma, kibao wala kitu kingine. Imethibiti kutoka kwa Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) kupitia Hadiyth ya Jaabir (Radhiya Allaahu ´anh) kwamba:

“Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amekataza kulitia chokaa kaburi, kukaa juu yake na kujenga juu yake.”

Ameipokea Imaam Muslim katika “as-Swahiyh” yake. at-Tirmidhiy na an-Nasaa´iy wamezidisha kwa cheni ya wapokezi Swahiyh:

“Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amekataza kulitia chokaa kaburi, kukaa juu yake na kujenga juu yake na kuandika juu yake.”

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Majmuu´-ul-Fataawaa (09/378)
  • Imechapishwa: 24/07/2021