Haifai kwa mwanamke kuchanganyikana na wanamme mahali kokote

Swali: Ni zipi nasaha zako juu ya zile shubuha zinazotokea katika jamii kuhusu kutoka nje kwa mwanamke na kuchanganyikana kwake na wanamme katika maeneo ya kazi, maeneo ya mazoezi na kwengineko?

Jibu: Haijuzu kwa mwanamke kuchanganyikana na wanamme mahali kokote; si kazini, sokoni, mazoezi wala kwenginepo. Haya ni maovu. Ni lazima kwa mwanamke kuwa mbali na wanamme. Ikiwa mwanamke katika swalah na ´ibaadah nyenginezo anakuwa nyuma ya wanamme, tusemeje ikiwa mchanganyiko unatokea kazini na maeneo mengine ambapo hukusanyika na wanamme? Yote haya ni maovu. Ni lazima kwa wasimamizi kulizingatia jambo hili na watekeleze kile walichosimamia na wawakataze wanawake wao suala la mchanganyiko. Ni mamoja hayo yanafanyika kazini au maeneo mengine ambapo hukusanyika na wanamme.

  • Mhusika: ´Allaamah ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah ar-Raajihiy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Fataawaa Mutanawwi´ah (21)
  • Imechapishwa: 10/09/2021