Haifai kuwahudumia makafiri chakula mchana wa Ramadhaan

Swali: Mtu huyu alikuwa anataka kujua kama anapata dhambi kwa kuwahudumia chakula makafiri mchana wa Ramadhaan?

Jibu: Haijuzu kuwahudumia chakula wakiwa sio waislamu na wakataka kuhudumiwa chakula Ramadhaan. Mtu asifanye hivo na akawasaidia juu ya jambo hilo ijapokuwa wao ni makafiri na haisihi kwako kufunga. Lakini wao ni wenye kuguswa na mataga ya Shari´ah. Wakiwa ni wenye kuguswa si sawa kuwasaidia katika mambo yanayoenda kinyume na Shari´ah. Bali wanatakiwa kunasihiwa na kuelekezwa kwani huenda wakaingia katika Uislamu na mtu akapata mfano wa ujira wao:

“Yule mwenye kuelekeza katika kheri anapata ujira mfano wa yule mwenye kuifanya.”

“Allaah kukuongozea mtu mmoja ni bora kwako kuliko ngamia wekundu.”

Hivi ndivyo amesema Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam).

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: https://www.youtube.com/watch?v=b31JsAUehuM
  • Imechapishwa: 22/05/2018