Swali: Inafaa kumpelekea mtoto wa Kiislamu akanyonyeshwe au akalelewe na mwanamke mlezi wa kafiri[1]?

Jibu: Haijuzu kumuweka mtoto pamoja na mwanamke wa kikafiri. Kwa sababu atamlea juu ya dini yake. Lililo la wajibu ni kutilia umuhimu suala la watoto wa Kiislamu. Haitakiwi kuwaacha pamoja na wanawake wa kikafiri.

Leo kwa masikitiko makubwa watu wengi wanaagiza wanafanyakazi wa kikafiri. Unawaona wanawake wanaenda na wanawaacha watoto wao pamoja na hawa wanawake wa kikafiri ambapo wanawake hawa wanawafunza dini yao. Tunasikia kwamba baadhi ya watoto ambao wamelelewa na hawa wanapoulizwa kuhusu mungu wao wanasema kwamba ni ´Iysaa. Kwa sababu ambaye kawalea ni mnaswara. Haya ni majanga na mabalaa. Hili ni kwa sababu watu wengi wamejishughulisha na dunia na wakaacha kuwalea watoto wao. Dunia imekuwa ndio yenye kutangulizwa.

Ni wajibu kwa mtu atilie umuhimu juu ya watoto wao, akawaelee na kuwafunza. Haijuzu kwa mtu kuleta wafanyakazi wa kike na wa kiume makafiri. Hili halifai likatendwa katika kisiwa cha kiarabu. Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:

“Waondosheni mayahudi na manaswara katika kisiwa cha kiarabu.”

“Kusibaki katika kisiwa cha kiarabu dini mbili.”

Ni wajibu kwake kutumia wafanya kazi wanaume au wanawake. Hata mfanyakazi wa kike inapaswa kwa mtu amtumie pamoja na Mahram wake. Haijuzu kwa bosi wake kukaa naye faragha wala yeyote katika watoto wa kiume wa bosi.

Watu wengi utawaona ima wao au watoto wao wa kiume wanakaa faragha na wafanya kazi wa kike kwenye gari. Wakati mwingine utaona vilevile mfanya kazi wa kiume anapanda gari peke yake na mwanamke au anaingia mahali wanawake wako wanapika. Matokeo yake anachanganyikana na wanawake. Haya hayajuzu. Yote haya ni miongoni mwa sababu zinazopelekea katika machafu.

Ni wajibu mfanya kazi wa kiume awe pamoja na wanaume wenzake na mfanya kazi wa kike awe pamoja na wanawake wenzake. Kusiwepo mchanganyikano hawa kwa hawa wala yeyote katika watoto wao. Kila wamoja wawe upande wao.

[1] Tazama https://firqatunnajia.com/watoto-wa-kiislamu-kwenye-chekechea-daycare-nursery-school-za-kikafiri/ 

  • Mhusika: ´Allaamah ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah ar-Raajihiy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Fataawaa Mutanawwi´ah (04) http://audio.islamweb.net/audio/index.php?page=FullContent&audioid=191047#191047
  • Imechapishwa: 01/09/2018