Haifai kuitoa swalah nje ya wakati wake

Swali: Sisi ni wanafunzi ambao tunasoma sekondari ambayo iko mbali na kijiji chetu karibu 13 km. Tunaelekea shuleni karibu saa 01.00 wakati wa adhuhuri na hatufiki katika kijiji isipokuwa karibu saa 02.00 baada ya adhuhuri. Je, inajuzu kwetu kuswali Dhuhr papo kwa hapo baada ya kufika au tuikidhi pamoja na ´Aswr?

Jibu: Ni wajibu kwenu kuswali Dhuhr kabla ya kuanza safari, baada ya kusafiri au wakati wa safari. Msicheleweshe mpaka wakati wa alasiri. Ni wajibu muiswali ndani ya wakati. Mkiiswali kabla ya hapo wakati mtapokuwa masomoni mkajitajidi kuswali mwanzoni mwa wakati basi hivyo ndio bora. Jengine mnaweza kuswali njiani au mkaswali mjini mwenu. Kwa sababu kuswali mwanzoni mwa wakati ndio bora.

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziy bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Fataawaa Nuur ´alaad-Darb http://www.alifta.net/Fatawa/fatawaChapters.aspx?languagename=ar&View=Page&PageID=1238&PageNo=1&BookID=5
  • Imechapishwa: 15/03/2018